HabariMazingiraNews

NEMA yawahimiza wakaazi Kwale kupanda miti…….

Mamlaka ya mazingira nchini (NEMA) imewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kupanda miti kwa wingi ili kuafikia asilimia 10 ya idadi ya misitu nchini.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kaunti ya Kwale Godfrey Wafula amewataka wakaazi wanaoishi katika maeneo ya Kinango na Lungalunga kuzingatia upanzi wa miti hiyo.

Kulingana na Wafula, idadi ya misitu katika maeneo hayo ingali iko chini mno kutokana na uhaba wa mvua na ukataji wa miti kiholela.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya mazingira kaunti ya Kwale Joseph Indo amesema kaunti hiyo iko na kiwango cha asilimia 6.7 ya idadi ya misitu nchini.

Aidha, Indo amedokeza kwamba tayari wamepanda miti elfu 75 katika mashamba ya wakulima na shule mbali mbali kaunti hiyo.

By Kwale Correspondent