HabariNewsTravel

Juhudi za uokoaji zinaendelea kufuatia kuanguka kwa ndege ya jeshi la ulinzi nchini KDF…

Juhudi za uokoaji zinaendelea kufuatia kuanguka kwa ndege ya jeshi la ulinzi nchini KDF katika eneo la Ol Tepesi kwenye kaunti ya Kajiado.

Ndege hiyo imeanguka mwendo wa saa tatu asubuhi hii ilipokuwa kwenye mafunzo na inahofiwa kwamba abiria wot 23 waliokuwa ndani yake wameaga dunia.

Msemaji wa KDF Zipporah Kioko amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akisema taarifa ya kina itatolewa wakato wowote.

Ndege hiyo ya MI 171E imeanguka na kushika moto ikiwa na watu hao 23.

Maafisa kadhaa wa usalama tayari wamefika katika eneo la tukio.

BY WARDA AHMED