HabariKimataifaNews

Shirika La Kimataifa La Mikopo  (IMF) limetoa mkopo wa awamu ya pili kwa taifa  la Kenya…

Shirika La Kimataifa La Mikopo  (IMF) limetoa mkopo wa awamu ya pili kwa taifa  la Kenya wa takriban shillingi billioni 44 kutoka mkopo wa shillingi billioni 252 uliombwa na Kenya.

Mwenyekiti wa bodi la shirika hilo  Antoinette Sayeh amesema kuwa fedha hizo zitasaidia Kenya kugharamia madeni pamoja na kukabiliana na virusi vya Corona .

Aidha amehimiza serikali kuweka  mikakati na sheria ambazo zitasaidia taifa hili kukusanya  mapato zaidi ili kuimarisha maisha ya wananchi pamoja na kufanya maendeleo ya miundo msingi.

Kwa wakati huo Rais Uhuru Kenyatta amepongeza hatua hiyo na kuwasihi wale ambao wanakashifu hatua ya serikali yake kutokana na kuchukua mikopo mingi kuelewa kwanza ni kwanini mikopo hii huchukuliwa.

NA WARDA AHMED