HabariNews

Taita Taveta yapata afueni baada ya maafisa 31 kuhitimu kuwa wazima moto….

Ni afueni kwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta baada ya maafisa 31 kukamilisha mafunzo yao ya mwezi mmoja na kuhitimu kuwa wazima moto.

Mafunzo hayo yaliongozwa na maafisa kutoka shirika la mamlaka ya Bandari nchini KPA  haya yanajiri baada ya serikali ya kaunti hiyo kununua magari mawili ya kuzima moto  yanayodaiwa kugharimu kaunti hiyo zaidi ya shilingi milioni 20.

Wafanyibiashara hasa mjini wamekuwa wakilalamika kuwa kaunti haikuchukuwa hatua za kukabiliana na visa vya moto vinapotokea .

Aidha washikadau wamezipongeza idara husika kwa kuwezesha mafunzo hayo huku sasa wakiwa na matumaini kuwa mikasa hiyo haitokuwa kero kwa jamii tena.