HabariNews

KRA kuongoza mnada wa bidhaa zilizokaa bandarini kwa muda…….

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA leo na kesho inatarajiwa kuongoza shughuli ya kuyapiga mnada magari 315 na bidhaa nyingine katika bandari ya KPA hapa mjini Mombasa.

Mshirikishi wa mamlaka hiyo eneo la Kusini Joseph Tunui amesema bidhaa nyingine ambazo ziko ndani ya makasha 223 ni nguo na viatu zilizotumiwa.

Wakati huo huo amesema wananchi wanaotaka watapewa nafasi ya kushiriki kwenye mnada huo, huku akisema shughuli hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia masharti yote ya kukabili maambukizi ya corona.

KRA inalenga kukusanya kati ya shilingi milioni 150 na 200 kutoka kwa mnada wa bidhaa hizo ambazo zimekawia bandarini baada ya kupitisha muda unaofaa wa bidhaa zilizoagizwa nchini kuondolewa, ikiwemo waagizaji kushindwa kulipa kodi ya kiwnago kilichostahili.

By Warda Ahmed