HabariNewsSiasa

SIFUNA asema bado ODM ni chama cha upinzani…….

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amesisitiza kwamba bado chama hicho ni cha upinzani, na kinaendelea kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza katika mahojiano ya kituo kimoja cha radio, Sifuna ametumia mfano wa mabadiliko katika makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa bungeni hapo jana na kamati inayoongozwa na mwakilishi wa kike wa Homabay Gladys Wanga ambaye ni mwanachama sugu wa ODM.

Kuhusu muungano wa NASA, Sifuna ameregelea kauli kwamba muungano huo haupo na mwisho wake ulikuwa  mwaka 2018 wakati vinara wenza walisusia uapisho wa Raila Odinga kuwa rais wa wananchi.

By Warda Ahmed