HabariNewsSiasa

Mamlaka ya ajira yatakiwa kutafuta nafasi za ajira katika mataifa ya kigeni…..

Serikali kupitia wizara ya Leba imetoa agizo kwa mamlaka ya ajira nchini kutafuta nafasi 100,000 za ajira katika mataifa ya kigeni sawia na humu nchini ili kuokoa maelfu ya vijana wanaohangaika nchini kwa kukosa ajira.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa leba Simon Chelugui ambaye pia ametoa wito kwa vijana kujitokeza na kusomea kazi za kiufundi ili waweze kujiajiri.

Chelugui ameyazungumza haya akiwa katika kaunti ya Mombasa kwenye kikao kilichoandaliwa kuangazia changamoto za ajira nchini akiwarai vijana kuwajibika ili waweze kunufaika kutokana na mpango huo.

Aidha waziri huyo amesema kufikia sasa visa vya wakenya kuhangaishwa katika mataifa ya kigeni vinazidi kupungua kufuatia uhusiano mwema unaoendelea baina yao na mataifa tofauti humu nchini.

By Gladys Marura