AfyaHabariNews

Wito wa magavana kutaka kuruhusiwa kuagiza chanjo ya corona wakataliwa….

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amepuzilia mbali ombi la magavana la kutaka kuagiza chanjo ya Corona akisema kwamba taifa linapaswa kuhakikisha usalama wa chanjo zinazotolewa kwa raia wake.

Mutahi amesisitiza kuwa njia ni tatu tu za kupookea chanjo, ikiwa ni kutoka kwa serikali hadi serikali ingine, Shirika la kusambaza chanjo ya Corona ulimwenguni Covax na vituo mbalimbali vya umoja wa Afrika

Haya yanajiri huku taifa la Kenya likingojea kupokea chanjo ya Pfizer kutoka marekani.

By Warda Ahmed