Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion amejiuluzu kama katibu mkuu.
Akizungumza jijini Nairobi Sossion ambaye pia ni mbunge mteule amesema kwamba anajiuzulu kutoka kwa chama kwa faida na kuendelea kwa chama hicho.
Amesema kwamba atabaki kuwa mwanachama mwaminifu huku akiirai serikali ya kitaifa kutenga fedha zaidi kwa minajili ya kuboresha maisha ya waalimu na wafanyikazi wote wa umma.
Vilevile Sossion ameongeza kwamba ataendelea kuwahudumia wakenya kwa namna ingine akiongeza kuwa atajitolea kwa kazi yake bungeni hasa kuwapigania wafanyikazi wote nchini.
Haya yanajiri huku chama cha walimu KNUT kikitarajiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wapya hapo kesho katika uwanja wa Ruaraka jijini Nairobi.
Sossion amewataka wote watakaochaguliwa hapo kesho kuheshimu malengo ya tume hiyo akiwahimiza wasishawishiwe na mamlaka yeyote.
Sossion alichukuwa wadhfa wa ukatibu mkuu wa chama cha walimu KNUT mwaka 2013 baada ya kifo cha aliyekuwa katibu mkuu David Okuta.
By Joyce Kelly