Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho amewaonya baadhi ya wakaazi wanaounganisha mabomba bandia ya maji taka kinyume cha sheria katika mtaa wa Mji wa kale hapa Mombasa.
Akizungumza alipozuru mradi wa ukarabati wa mabomba mapya ya maji taka mtaani humo,Joho amesema kunao baadhi ya wakaazi mtaani humo wanaounganisha mabomba yao ya maji taka kinyume cha sheria hali ambayo imechangia pakubwa kutapakaa kwa maji hayo mitaani.
Kadhalika Joho amewataka wakaazi wa mtaa huo kubeba majukumu yao kikamilifi na kuhakikisha kuwa wanaepuka kutupa taka kiholela kwenye mabomba ya maji taka.
Wakati huo huo mbunge wa Mvita ABdulswamad Shariff Nassir ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kuandaa kampeni ya uhamasisho kwa wakaazi wa mtaa huo kuhusiana na umuhimu wa kutokuwepo kwa mabomba yaliyojengwa kinyume cha sharia.
Aidha ukarabati wa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi huu.
By Reporter