HabariNewsSiasa

DAN ALOO AWAKASHIFU WABUNGE …

Mgomea wa kiti cha ubunge wa jomvu Dan Aloo amekashifu vikali hatua ya baadhi ya wabunge kutaka kumngatua mamlakani waziri wa usalama wa ndani Dr fred Matiangi akisema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa viongozi hao hawana haja na uongozi bora.

Akizungumza na meza yetu ya habari katika mahojiano ya kipekee kiongozi huyo amesema kuwa waziri matiangi ni moja wapo wa mawaziri katika serikali ya rais kenyatta ambao wanafanya kazi ipasavyo hivyo basi badala ya kumngatua mamlakani wabunge hao wangechukulia hatua naibu wa rais.

Wakati huo huo ametoa wito kwa wabunge kutoka mirengo ya chama cha ODM na jubilee kutupulia mbali mswada huo wa kutaka matiangi kuondolewa.

BY DAVID OTIENO.