HabariNewsSports

RAIS UHURU KENYATTA AZINDUA KIKOSI KITAKACHOWASILISHA KENYA KWA MASHINDANO YA OLIMPIKI MJINI TOKYO…

Rais Uhuru Kenyatta amekizindua rasmi kikosi cha wanariadha watakaowakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki ambayo yatang’oa nanga tarehe 23 mwezi huu mjini Tokya Japan.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta anekihimiza kikosi hicho kudumisha hadhi ya Kenya katika mashindano hyo.

Aidha amekihimizi kushirikiana na kuiletea Kenya fahari kupitia mashindano hayo.

Aidha rais Kenyatta amesema kwamba serikali yake itaendelea kuwekeza hata zaidi kwenye tasnia ya michezo ili kukuza talanta miongoni mwa vijana.

Haya yanajiri masaa machache baada ya waziri mkuu wa Japan Suga kutangaza hali tarehe katika taifa hilo kuanzia tarehe 12 mwezi huu hadi Agosti 22 mwaka huu.

Hata hivyo mashindano hayo ya olimpiki yatafanyika ila chini hatua zilizoekwa za dharura.

. BY JOYCE MWENDWA