HabariSiasa

UKOSEFU WA USHAHIDI KUATHIRI KESI ZA MAUAJI YA KIHOLELA …

Ukosefu wa ushahidi wa kutosha umetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazoathiri pakubwa kesi zinazohusu mauaji ya kiholela.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji anayesema kuwa hatua hiyo imeathiri mchakato wa kutafuta haki mahakamani.

Akizungumza katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, Haji amesema kuwa upasuaji wa maiti ni muhimu katika uchunguzi wa kesi hizo.

Kwa upande wake afisa wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Hussein Khalid amesema kuwa kesi nyingi hazijatatuliwa kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Khalid amesema kwamba upasuaji wa maiti utasaidia katika ushahidi wa kesi hizo ili kuhakikisha waathiriwa wanapata haki.

Haya yanajiri katika kikao kilichowaleta pamoja viongozi wa kidini na watetezi wa haki kujadili swala la upasuaji wa maiti kwa waislamu.

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED