HabariMombasaNews

VIONGOZI ENEO LA PWANI WATAKIWA KUACHA HISTORIA ….

Huku ikiwa imesalia mwaka mmoja kwa hatamu za viongozi wengi kukamilika hasaa magavana eneo la Pwani,wakaazi wa eneo la Pwani wamewataka viongozi hao kuacha historia katika utendakazi wao na wala sio kuwanyanyasa.

Wakiongea na meza yetu ya habari ,wakaazi hao wameanza kuwa na wasiwasi na hatua za baadhi ya viongzi ambao wamekamilisha muda wao wa kuhudumu, kutokana na kuzembea kwao katika kuangazia maslahi ya wananchi.

Aidha wamewaomba viongozi hao hasaa wabunge kutumia nafasi ambayo wamepewa kikatiba kuangalia maswala mbalimbali yanayowatatiza wakaazi wanamoishi katika maeneo mbalimbali katika kaunti ya Mombasa.

BY PRESTON WANDERA