HabariMombasa

KUNA HAJA YA SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA KUWEKA MIKAKATI KUONA KUWA VISA VYA MOTO VINAKABILIWA …

Kuna haja ya serikali ya kaunti Mombasa kuweka mikakati ili kuona kuwa visa vinavyoshudiwa vya kuzuka kwa moto katika maeneo ya soko hapa Mombasa vinakabiliwa.

Haya ni kwa mjibu wa mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir.

Ameyasema haya baada ya maduka 20 ya nguo katika soko la Marikiti hapa Mombasa kuteketea, ikiwa ni siku chache baada ya kushudiwa kwa tukio lingine la moto katika sehemu ya soko kuu la Kongewea.

Akizungumza hii leo na waathiriwa wa mkasa huo Abdulswamad amewataka waathiriwa hao kuwa na subra huku wakiwa katika harakati ya kutafuta suluhu mwafaka si kwa mkasa wa eneo hilo pekee bali suluhu la kukabili kuibuka kwa moto katika maeneo mbali mbali ya ndani ya kaunti.

Aidha amesema kuna haja ya kuundwa kwa jopo kazi ili kukabiliana na majanga ya moto.

Jumla ya maduka 20 ya nguo yameteketea huku hitilafu za umeme ikitajwa kama chanzo kikuu cha kuzuka kwa moto huo.

BY REPORTER