HabariNewsSiasa

WAKAAZI KAUNTI YA KILIFI WAONYWA DHIDI YA KUENEZA UVUMI…

Huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo kilichopele  kea mauwaji ya watu watatu kwa tuhuma za utekaji nyara wa watoto huko Junju katika kaunti ya Kilifi, kamati ya usalama katika kaunti hio imewaonya wakaazi dhidi ya kueneza uvumi kuhusiana na utekwaji nyara.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati ya usalama kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka, amekemea kitendo hicho na kukitaja kama kitendo kisichofaa katika jamii.

Olaka aidha ameongezea kwamba wanachi hawana ruhusa ya kuchukulia sheria mikononi na badala yake kupiga ripoti kwa vyombo vya usalama iwapo wanatilia shaka kuhusiana na tukio lolote.

Wakati huo huo, mwenyekiti huyo amewahakikishia wakaazi wa Kilifi usalama wa kutosha huku akiwataka kupuuzilia mbali dhana ya utekwaji nyara wa watoto.

BY NICK WAITA