AfyaHabari

CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA POLIO KUANZA TAREHE 17 WIKI HII KAUNTI YA MOMBASA

Wito umetolewa kwa wenyeji wa kaunti ya mombasa kujitokeza na watoto wao wenye umri wa chini ya miaka mitano kupokea chanjo ya ugonjwa wa polio itakayonza tarehe 17 wiki hii.Akizungumza na meza yetu ya habari baada ya kuandaa mkutano wa kuhamasisha washidau mbali mbali ikiwemo chifu na maibu wao afisa ya afya umma katika kaunti ndogo ya mvita Oliver Oluoch amewasihi wazazi kuhurusu watoto wao kuchanjwa na kueka kando dhana potovu.Wakati huo huo afisa huyo amesema kuwa chanjo hiyo ni salama kwa afya ya kila mtoto hivyo basi kila mmoja anapswa kuruhusu mwanawe kupokea chanjo pasi na kujali maoni ya watu ambao wanatoa dhana mbaya kuhusiana na  zoezi hilo.

 

BY DAVID OTIENO