Habari

SERIKALI KUMALIZA UKEKETAJI NCHINI IFIKIAPO MWAKA WA 2022

Serikali inapania kumaliza ukeketaji katika kaunti zote humu nchini ifikiapo mwaka wa 2022 kulingana na miundo msingi iliyowekwa kwa kaunti tofauti tofauti.

Akizungumza mjini Narok baada ya uziduzi rasmi wa muongozo dhidi ya ukeketaji, mkurungenzi wa idara ya jinsia Agnes Ngw’eno amesema kuwa idara hiyo itashirikiana na serikali katika kumaliza ukeketaji hasa kwa vijana wadogo na pia kuwaelimisha kupitia kwa mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo, serikali imezidua sera za kukabiliana na ukeketaji huko Narok na kusema kuwa mikakati zaidi itawekwa ili kumaliza visa hivyo kote nchini na pia kuchukulia mkono wa sheria wanaoendeleza visa vya ukeketaji.

 

BY CAROLINA NYAKIO