HabariSiasa

Kingi Awaonya Wanasiasa dhidi ya kutumia swala la mzozo wa ardhi kuwachochea wanainchi……………..

Gavana wa Kilifi Amason Kingi amewaonya wanasiasa dhidi ya kutumia swala la mzozo wa ardhi katika kaunti hiyo kuwachochea wakazi.

Akizungumza mjini Kilifi, Kingi amesema hatua ya viongozi wa kisiasa kuwachochea wakazi kuzua fujo ni jambo la kihalifu ambalo litakabiliwa kisheria.

Aidha amewataka viongozi kukoma kuchochea wakazi katika maswala ya ardhi kwa manufaa yao binafsi hasa wakati huu ambapo viongozi wa kisiasa wanaendelea kuweka mikakati ya kuimarisha kampeni ili kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2022.

Aidha amewaonya wakazi ambao wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kuzua fujo kwamba sheria itakabiliana nao, huku akiwataka kukoma kuvamia mashamba ya watu na kuyafanya makazi yao.

Kingi ameongeza kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi inashughulikia kutatua mizozo ya ardhi katika kaunti hiyo ili kila mkaazi apate haki ya kumiliki ardhi.

Ikumbukwe swala la mzozo wa ardhi kaunti ya Kilifi na ukanda wa pwani kwa jumla limekuwa likitatiza na halijapata suluhu ya kudumu mpaka kufikia sasa.