HabariSiasa

ANC YAANZA MIKAKATI YA KUTAFUTA UUNGWAJI MKONO KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

Chama cha Amani National Congress ANC kimeanza mikakati yake ya kutafuta uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kulingana na seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala, jukumu la viongozi wa vyama vya kisiasa ni  kuwaunganisha wakenya badala ya kufanya siasa za mgawanyiko.

Akizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini Kilifi baada ya kukutana na viongozi walionyesha nia ya kugombea nyadhifa za uongozi kupitia chama hicho, Malala amesema chama cha ANC kinaendelea kuwasajili wanachama wake ili kujiweka tayari kwa uchunguzi mkuu wa mwaka ujao wa 2022.

Aidha ameongeza kuwa muungano wa ONE KENYA ALLIANCE umefungua milango yake kwa viongozi wanaotaka kujiunga na muungano huo ili kuimarisha muungano huo wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Kwa upande wake naibu mwenyekiti wa chama hicho aliyepia mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza  amesema kinara wa chama hicho Musalia Mudavadi anatarajiwa kuzuru kaunti za ukanda wa pwani kuanzia tarehe 26 mwezi huu wa Julai kutafuta uungwaji mkono.

 

BY ERICKSON KADZEHA