Gavana wa Migori Okoth Obado ndiye baba mzazi wa mtoto wa marehemu Sharon Otieno aliyeuawa kwa kudungwa kisu akiwa tumboni mwa mamake.
Akitoa ushahidi wake hii leo kwenye kesi ya mauaji ya Sharon, John Kimani Mungai ambaye ni mkaguzi wa maiti katika maabara ya serikali, amesema chembechembe za DNA zilizochukuliwa kutoka kwa Obado zilifanana kwa asilimia 99.9 na mtoto wa Sharon.
Kulingana na Mungai mbegu za kiume zilizopatikana kwenye kondomu iliyopatikana kwenye eneo la tukio ilibainika ni ya mwanamume asiyejulikana
Aidha ameongeza kwamba Michael Oyamo ambaye ni msaidizi wa gavana Obado si baba mzazi wa mtoto wa marehemu Sharon.
BY JOYCE MWENDWA