Habari

Magoha Awaonya vikali waalimu dhidi ya kuwaregesha wanafunzi nyumani kwa kukosa karo…………………

Waziri wa elimu nchini Profesa George Magoha amewaonya vikali walimu wakuu katika shule za upili dhidi ya kuwaregesha wanafunzi nyumbani kwa kukosa kulipa karo.

Waziri huyo amesema wazazi ambao bado hawajalipa ama kumaliza malipo ya karo kupewa muda zaidi iki kukamilisha karo hizo kwani kuwatoa watoto darasani kwasababu ya karo kutaathira sana masomo ya wanafunzi .

Akizungumza katika shule ya msingi ya Motuma Gatundu Kusini kaunti ya Kiambu wakati wa kutoa ufadhili kutoka  kwa Ahadi Kenya kwa minajili ya kujikinga kutokana na virusi vya korona ,Magoha amesema tayari serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 59.4 kwa shule za upili.

 

By News Desk