Habari

Wafanya Biashara katika mpaka wa Kenya na Tanzania walalamikia kunyanyaswa na maafisa wa polisi wa Tanzania……….

Wafanyibiashara wanaohudumu katika mpaka wa Kenya na Tanzania katika eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale wamelalamikia kunyanyaswa na maafisa wa polisi wa Tanzania.

Wakiongozwa na Rosemary Nyaga, wamedai kwamba maafisa hao wanawanyanyasa kwa kuzuia bidhaa zao mpakani mbali na kuwahangaisha barabarani.

Wafanyibiashara hao pia wamedai kuwa machifu wanaoshirikiana na maafisa hao wanawaitisha hongo kabla ya kuwaruhusu kuingiza bidhaa zao nchini.