HabariSiasa

HAZINA YA MAENDELEO BUNGE YA KILIFI KASKAZINI KUTOA BASARI

Viwango ya umaskini vikiendelea kupanda na kutatiza maswala ya elimu katika eneo bunge la Kilifi kaskazini, hakikisho limetolewa kwa wakazi wa eneo bunge hilo kuwa ufadhili wa masomo utatolewa hivi karibuni.

Kulingana na mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya wanafunzi wengi wamekosa nafasi katika mpango wa Wings To Fly na elimu Scolarship kuwawezesha kujiunga  na kidato cha kwanza  ilhali umasikini katika eneo bunge hilo ni wa kiwango cha juu.

Baya amesema hazina ya eneo bunge ya NG-CDF itaoa basari kwa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha cha kwanza wiki ijayo ,ikilenga wale ambao wamekosa ufadhili wa mashirika mbalimbali huku akitoa shukrani zake kwa benki ya Equity na mashirikia yasiyokuwa ya serikali kuchukua hatua ya kusaidia watoto masikini

Aidha amesema ametenga  takribani shilingi  milioni 4.2 za kuwafadhili wanafunzi ambao watajiunga na kidato cha kwanza huku akiongeza kuwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao watanufaika na kitika cha shilingi milioni 3.

 

BY ERICKSON KADZEHA