Waziri wa afya Mutahi Kagwe ameagiza mamlka ya usambazaji dawa nchini KEMSA kuviuza vifaa vyote vya kukabili maradhi ya Corona vinavyohifadhiwa katika mabohari ya mamlaka hiyo.
Kagwe amesema kuviuza vifaa hivyo kabla ya muda wake kuharibika kufika, itaisaidia serikali kutopotea takribani shilingi bilioni 19.
Katibu mkuu msimamizi katika wizara ya afya Daktari Mercy Mwangangi amesema kwamba watu wenye magonjwa yasiyoambukizwa watapewa kipaumbele kwenye awamu ya pili ya utoaji wa chanjo.
Amezungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati wa miaka mitano kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa ambao utatekelezwa kuanzia mwaka huu wa 2021 hadi 2026.
Aidha amesema kwamba asilimia 39 ya watu ambao huugua magonjwa hayo huaga dunia kila mwaka na kuwa idadi hiyo imeongezeka.
BY REPORTER