HabariSiasa

Ruto aunga mkono kutengwa na serikali ya jubilee……..

Naibu rais William Ruto ameunga mkono kwamba ametengwa na serikali ya jubilee, akisema majukumu yake yote sasa yamepewa waaziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi tangu kulipofanywa salamu za maridhiano maarufu Handshake.

Akihojiwa na kituo kimoja cha radio humu nchini, Ruto amesema kupitia handshake, serikali ilikorogeka na ajenda ya big 4 haikupewa tena kipau mbele kwani suala la kufanyia katiba marekebisho kupitia BBI lilipewa uzito zaidi na upinzani.

Ruto aidha amesema kwamba hatua hiyo ilifanya majukumu yake yote kupewa waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi.

Kuhusu ziara zake nchini Uganda,  Ruto amesema rais wa Uganda Yoweri Museveni ni rafiki wa rais Uhuru Kenyatta na pia ni rafiki yake akisema aliwahi kumfanyia kampeni nchini Uganda wakati wa uchaguzi mkuu akisema hakuna makosa yoyote kushirikiana na Museveni.

 

By news desk