HabariSiasa

Ruto autetea vikali mfumo wa Bottom up economic model……..

Naibu rais William Ruto ameutetea vikali mfumo wa kuinua uchumi kuanzia ngazi wa chini wa bottom up economic model, ambao unaendelea kupingwa vikali na washindani wake wa kisiasa.

Akihojiwa na radio ya Inoro, Ruto amesema bottom up ndio njia pekee ya kuwakwamua wananchi wenye matabaka ya chini, baada ya asilimia kubwa na wananchi kuundelea kuathirika kufuatia kudorora kwa uchumi hswa vijana.

Wakati huo huo Ruto amewakosoa wale wote wanaosema kwamba hana jipya la kuwaahidi wakenya kwani amekuwa naibu wa rais chini ya serikali ya jubilee na hivyo anapaswa kuondoka baada ya mihula miwili kwa kukosa kutimiza ahadi walizotoa kwa wakenya ikiwemo ile ya big 4.

Ruto aidha amesema iwapo atachaguliwa kuwa rais wa taifa hili hatomtenga naibu wake akitaka afisi ya rais ipewe heshima pamoja na katiba.

Kuhusiana na uhusiano wake na mfanyabishara Harun Aydin ambaye ni raia wa Uturuki naibu rais amekinzana na wanaodai ni mhalifu wa kimataifa akisema kuwa Aydin ni mwekezaji na amekua akisafiri humu nchini mara kwa mara kujaribu kuwekeza kwenye biashara ya ukulima.

 

By News desk