Habari

Mzozo watotokota kuhusu usimamizi wa shule ya upili ya Mambrui…..

Baadhi ya wakaazi wa Mamrui eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanalaumu wasimamzi wa shule ya upili ya Mamrui kwa kuisajili kama shule ya kibinafsi.

Kulingana na wakaazi shule hiyo ilianzishwa mwaka 2003 na wazazi waliochanga shilingi 2000 kila mmoja na kujenga baadhi ya majengo shuleni humo na baadaye wafadhili walitoa msaada wa kuiboresha shule hiyo.

Wakaazi hao wanasema kipande cha ardhi ilipojengwa shule hiyo kilitolewa na jamii na wanashangaa kwanini sasa imesajiliwa kama shule ya kibinafsi.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Halima Omari alikiri kuwa shule hiyo imesajiliwa kama shule ya kibinafsi na kuongozwa na wadhamini jambo ambalo wakaazi wanapinga.

Stakabadhi kutoka afisi ya elimu Kilifi zinaonyesha kuwa shule hiyo ni ya kibinafsi.

 

BY JOYCE MWENDWA