AfyaHabariNews

Ushirikiano wahimizwa kukabili utumizi wa mihadarati miongoni mwa wanafunzi….

Wito umetolewa kwa wazazi na walimu kushirikiana ili kukabiliana na visa vya utumizi wa mihadarati miongoni mwa watoto wa shule.

Mwenyekiti wa shirika la Sauti ya wanawake katika eneo bunge la Matuga Mwanakombo Jarumani amewataka wazazi kushirikiana na walimu ili kuvikabili visa hivyo.

Jarumani amesema kuwa ushirikiano huo utahakikisha kuna nidhamu miongoni mwa wanafunzi ili wasiweze kushawishiwa.

Ni kauli iliyoungwa mkono na mkurugenzi wa Kwale Madrasa Teachers Sheikh Juma Lomba anayewataka pia wazazi kushirikiana na walimu wa madrasa.

Sheikh Lomba amewataka wazazi kutowatetea wanao wanaotumia dawa za kulevya ili kukomesha tabia hiyo.

By Kwale Correspondent