HabariNewsSiasa

TUME YA UWIANO NA MARIDHIANO NCHINI YAPENDEKEZA KUPEWA NGUVU ZAIDI ….

Tume ya uwiano na maridhiano nchini imependekeza kupewa nguvu zaidi za kuwafungulia mashtaka wanasiasa ambao hutoa matamshi ya chuki na vilevile wakitaka viongozi wa aina hio kuzuiwa kushiriki katika uchaguzi wowote ule nchini.

Mwenyekiti wa tume hiyo  Samuel Kobia amesema kuwa kesi zozote zitakazowakilishwa mbele ya mahakama zinapswa kusikizwa chini ya miezi sita .

Kobia amesema kuwa hatua hii itawasaidia kutekeleza majukumu yao kama inavyohitajika kwani mara nyingi wamesutwa kwa kuzembea kazini akisema sababu kuu ni kwamba hawakupewa mamlaka kama ya kuwafungulia mashtaka viongozi kama hao na katiba ya mwaka wa elfu mbili na kumi.

Haya yamejiri wakati wa kikao cha siku tatu  na kamati ya uwiano na nafasi sawa katika bunge la kitaifa wakati kumesalia na mwaka mmoja uchaguzi mkuu uandaliwe.

BY PRESTON WANDERA