HabariKimataifaWorld

Machafuko na mkanganyiko yashuhudiwa uwanja wa ndege wa Kabul…

Wanajeshi wa Marekani walipiga risasi hewani katika uwanja wa ndege wa Kabul, kulingana na AFP, wakati maelfu ya raia wa Afghanistan wakiwa wamekusanyika katika eneo la kuingia kwenye ndege tayari kutoroka Afghanistan.

“Ninahisi hofu sana hapa. Wanapiga risasi nyingi hewani”, mtu mmoja aliyeshududia tukio hilo ameliambia gazeti la AFP.

Video kadhaa zimeibuka za watu wanaokimbia katika barabara za uwanja wa ndege wakijaribu kupanda ndege.

Kuna ripoti kwamba ndege za Marekani zilizobeba wafanyikazi wa kidiplomasia kuwaondoa nchini humo, ndizo zilizopewa kipaumbele na kusababisha hasira, machafuko na mkanganyiko zaidi.

BY NEWS DESK