HabariMombasaNews

Zaidi ya familia 40 huko Nguu Tatu zabomolewa makaazi yao…..

Familia zaidi ya arobaini katika eneo la Nguu Tatu, Kisauni zimelazimika kukesha kwenye kibaridi kikali baada ya watu wasiojujikana na waliokuwa wameandamana na maafisa wa polisi kuvamia na kubomoa makaazi yao.

Inaarifiwa kuwa watu hao walivamia makaazi hayo mwendo wa saa nne usiku na kuanza ubomozi huo na kisha kutoweka na baadhi ya mali zao licha ya kesi ya kipande hicho cha ardhi kuwa mahakamani.

Aidha wakaazi hao wanasema kwamba mahakama ilikuwa imewapa idhini wakaazi kwenye ardhi hio hadi pale itakapotoa uamuzi wa kesi hio.

BY NEWS DESK