HabariLifestyleSiasa

Raila amepongeza Hichilema kwa kushinda uchaguzi Zambia….

Kinara wa ODM Raila Odinga amempongeza kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema kwa kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika wiki iliyopita nchini humo.

Hichilema amemshinda rais anayeondoka mamlakani Edga Lungu kwa zaidi ya kura milioni moja.

Katika taarifa hiyo, Raila ametaja hatua hiyo kama ukomavu wa demokrasia.

Haya yanajiri huku wafuasi wa Hichilema nchini Zambia wakiendelea kusherekea ushindi wake.

Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa usiku mzima baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza Hichilema kuwa mshindi.

BY NEWS DESK