Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amepinga madai kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kaunti hiyo wamekihama chama hicho.
Kulingana na Mwambire chama hicho hakijapokea barusa rasmi kutoka kwa viongozi ambao wanadai kukihama mwa mujibu wa taratibu za chama.
Akizungumza na vyombo vya habri kule Karimani wadi ya Bamba kwenye hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa madarasa mawili yalifadhiliwa na hazina ya maendelea ya NG-CDF, Mwambire amesema gavana wa kaunti ya Kilif Amason Kingi bado ni mwenyekiti wa chama hicho eneo bunge la Magarini.
Wakati uohuo Mwambire amemshukuru kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kwa kumpatia nafasi ya kuongoza chama hicho kaunti ya Kilifi.
Aidha Mwambire amesema ndani ya siku mia moja zijazo chama hicho kitaweka mikakati ya kuimarisha chama hicho hata zaidi ili kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Kauli ya mjumbe huyo inajiri baada ya chama hicho cha chungwa kumtimua Gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi kama mwenyekiti wa chama hicho kaunti hiyo kwa madai ya kupanga kuunda chama chengine eneo hilo.
By Malindi Correspondent