Serikali ya China sasa itawaruhusu wanandoa kuzaa watoto watatu, kwani inahofia taifa hilo kuwa na idadi ndogo ya watu hali itakayotishia mipango yake ya kukuza maendeleo na ushawishi ulimwenguni.
Bunge lilirekebisha sheria ya idadi ya watu na uzazi wa mpango, ikiwa ni miaka sita tangu mabadiliko ya mwisho yaliyoruhusu wazazi kuzaa watoto wawili.
Tangu miaka ya 1980 China ilikuwa ikiruhusu familia kuzaa mtoto mmoja tu.
Sheria hiyo ilisababisha baadhi ya wazazi kutoa mimba na wengine waliotaka mtoto huyo mmoja awe wa kiume wakiwaua watoto wao wa kike, hali iliyosababisha tofauti kubwa katika uwiano wa kijinsia nchini humo.
Japan na Ujerumani ni nchi nyingine tajiri zinazokabiliwa na changamoto sawa na hiyo ya kuwa na wafanyakazi wachache vijana na idadi kubwa ya wazee.
BY NEWS DESK