AfyaHabariNews

MADEREVA WA MASAFA MAREFU WANALALAMIKIA KUCHELEWESHWA KWA VIPIMO VYA VIRUSI VYA KORONA…….

Madereva wa masafa marefu wanalalamikia kucheleweshwa kwa vipimo vya virusi vya korona hatua inayosababisha kuchelewa kwa mizigo kutoka bandarini na kusafirishwa katika nchi mbalimbali.

Watu 1,166 wamepatikana na  ya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,924 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 230,794na kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.8%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 1,144 ni wakenya ilhali 22 ni raia wa kigeni,550 ni wanaume huku 616 wakiwa wanawake.

Kati ya maambukizi hayo mapya, kaunti ya Nairobi imeongeza kwa visa 347, Kiambu ina visa 208 huku Kajiado  ikiwa na visa 66.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 2, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 108.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 316wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,564 ya walioaga dunia.

Aidha watu 1,901 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 215,374, 1,699 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 202 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa2,013 ambao wamelazwa hospitalini,7,677 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 156 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

BY NEWS DESK