Naibu wa rais William Ruto amepuzilia mbali shinikizo la kutaka ajiunzulu kutoka kwa nafasi yake kufuatia kutofautina mara wa mara na rais Uhuru Kenyatta.
Kwa mara nyengine tena naibu wa rais William Ruto amedhihirisha kufurahishwa kwake na kuangushwa kwa mchakato wa mareebisho ya kikata kupitia kwa mswada wa bbi.
Akiongea huko Kwale wakati wa mazishi ya mamake gavana wa Kwale Salim Mvurya,Ruto anasema kwamba baadhi ya mapendekezo katika ripoti hiyo vingehujumu haki ya wakenya kwa kuingiliwa kwa idara huru ya Mahakama.
Kauli ya Ruto inajiri siku kadhaa tu baada ya baadhi ya Wabunge waliokuwa wakiunga mkono ripoti ya BBI kusema kuwa wataanzisha tena mchakato huo na kuusukuma bungeni.
Hatahivyo hisia mseto zimeanza kuibunga miongoni mwa Wakenya kufutia kauli za wabunge hao.
Baadhi ya wakenya tuliozungumza nao eneo hili la Pwani, wameonekana kuunga mkono swala hilo,wakisema kuna baadhi ya vipengee katika mswada huo vilikuwa vya manufaa kwa taifa.
BY NEWS DESK