Vijana kaunti ya Kwale wametakiwa kuwa wavumilivu hususan wanapotafuta ajira badala ya kukumbatia njia za mkato kupata hela.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa masuala ya vijana kaunti ya Kwale Kent Simiyu,amesema kuwa ukosefu wa subra kwa vijana kumewafanya kuingia katika maadili potovu.
Aidha Simiyu amewataka vijana kutafuta njia m’badala ya kujipatia fedha sababu njia hizo za mkato zina madhara makubwa baadae.
Mkurugenzi huyo amewashauri vijana kuachana na dhana ya kuajiriwa baada ya kufuzu kwani kazi siku hizi ni nadra sana kupata hivyo amewataka kubuni ujuzi kutokana na mafunzo hayo ya vyuoni na ufundi ili waweze kujiajiri wenyewe kama njia ya kujikimu kimaisha.
BY NEWS DESK