HabariNews

Magoha aendeleza oparesheni ya kuhakikisha wanafunzi wamejiunga na kidato cha kwanza……

Waziri wa elimu proffesa George Magoha hii leo anaendeleza oparesheni ya nyumba hadi nyumba katika kaunti ya Nairobi kuhakikisha kwamba asilimia 100 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE wamejiunga na shule za upili.

Magoha ambae ametoa makataa ya hadi ijumaa kwa wazazi kuwapeleka wana wao shuleni la sivyo wakamatwe, leo atapeleka oparesheni hiyo katika mitaa ya Dagoreti na Kangemi.

Akizungumza hapo jana katika kaunti ya Kiambu, Magoha alionya kwamba kufikia ijuma wiki hii polisi wataanza kuwakamata wazazi ambao hawatakuwa wamewapelekea wanao shuleni.

Oparesheni hii inaendelea huku idadi kubwa ya wazazi wakilalamikia changamoto mbali mbali ikiwemo umasikini, mimba za mapema ambazo zimewafanya wasichana kutojiunga na shule za upili na athari za corona miongoni mwa nyingine.

Hata hivyo athari kuu imetajwa kuwa kiwango cha karo kinachohitajika katika shule mbali mbali.

BY NEWSDESK