AfyaHabariNews

Serikali ya Mombasa yapokea dozi ya kwanza ya chanjo ya MODERNA……..

Serikali ya kaunti ya Mombasa imepokea awamu ya kwanza ya zaidi ya dozi elfu 11 za chanjo ya covid 19 aina ya Moderna.

Chanjo hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa hapo kesho  kwa watu wazima wenye zaidi ya miaka 18 na zaidi isipokuwa kwa wale ambao tayari wamepokea chanjo ya Astrazeneca.

Kulingana na taarifa ya afisaa wa mawasiliano wa serikali ya kaunti ya Mombasa Richard Chacha, chanjo hizo zitatolewa kupitia vituo vya afya ambavyo vimeidhinishwa.

Vituo hivyo ni Kliniki ya KPA, Zahanati ya Kaderbuoy, Kituo kikuu cha afya cha gereza la Shimo La Tewa, Hospitali ya Jocham, Hospitali ya Pandya, Hospitali ya Mombasa, Hospitali ya PREMIERE,Likoni vile – hospitali ya kaunti ya Tudor, Hospitali ya eneo la  Portreitz, Hospitali Kuu ya kutoa mafunzo ya Rufaa ya Ukanda wa Pwani (CGTRH).

Wananchi wa Mombasa wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kupata chanjo hiyo.

BY NEWS DESK