HabariMichezo

MASHINDANO YA SOKA KWA SHULE ZA UPILI ZA KIBINAFSI KUANZA IJUMAA YA TAREHE 10.09.2021

Mashindano ya soka kwa shule za upili zinazomilikiwa na watu binafsi yanatarajiwa kuanza ijumaa tarehe 10.09.2021 katika uwanja wa Anex ulioko Bamburi.
Takriban shule 12 zimethibitisha kushiriki kikuwe hiki na kugawanywa makundi manne.
Kundi A, kuna Mtwapa Starlight,Unda mshomoroni,New Hope na
Golden Chariot, huku kundi B, likiwa na Junda high,Mtwapa secondary,celebration high na Bahari.
Kwenye kundi C, kuna Valarye Macmilan,Junda Frere,Eaglewings, na Bedrock High, kisha D, limebeba,Coral high,Mtwapa Elite,Abstrard helping hands na Shanzu progressive
Mechi za ufunguzi zitakutanisha Mtwapa Starlight dhidi ya New hope
kisha Junda mshomoroni imalize udhia dhidi ya Golden Chariot.