AfyaHabariNewsSiasa

Ipo haja ya kutembelea vituo vya afya ili kujua afya yako kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu.

Wito umetolewa kwa wakazi wa Pwani na kenya kwa jumla kufika katika  vituo vya afya ili kupata vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu hasa msimu huu ambapo janga la korona limeathiri pakubwa taratibu za matibabu dhidi ya maradhi hayo.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee kwenye kipindi cha sauti asubuhi mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu katika kaunti ya mombasa kata ndogo ya nyali Rose Muthoka, ameshauri jamii kuangazia kwa uzito vipimo vya ugonjwa huo akidai kuwa ni hatari katika maisha ya kibanadamu hasa wakati huu ambapo virusi vya korona vimeathiri huduma za matatibu yake.

Muthoka anadai kuwa kutokana na ujio wa virusi hivyo wagonjwa wengi wanakosa kufika katika vituo vya afya kwa hofu ya kupata korona ama hata kuambiwa kwamba wanakorona jambo almbalo limethiri pakubwa vita dhidi ugonjwa huo.

Kwa upande Anne Nyambura ambae ni afisa kutoka shirika la Kelin linalotoa huduma za hamasa kuhusu ugonjwa huo ametoa wito kwa serikali kupitia idara ya afya kuwatengea waathiriwa wa TB chakula maalumu kama wanavyofanyimwa wagonjwa wengine.

Kwa upande wake Jerusha Ondu alieugua maradhi hayo hatari ya kifua kikuu amewasihi waathiriwa kufwata taratibu za matibabu hasa katika upande wa kumeza dawa akisema kuwa hiyo ndio njia pekee ya wao kupona ugonjwa huo.

BY DAVID OTIENO