AfyaHabari

Kenya yapokea dozi elfu 358 za chanjo ya Astrazenca kutoka Canada……..

Juhudi za serikali za kuwachanja wakenya dhidi ya covid 19 zinaendelea kuimarika baada ya Kenya kupokea dozi  elfu 358,000 mpya ya chanjo ya covid 19 ya astrazenca kutoka nchini Canada asubuhi ya leo ili kusaidia vita dhidi ya virusi  vya korona nchini.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa JKIA wakati wa kupokea dozi hizo akiwa na maafisa wengine wa afya, katibu mkuu katika wizara ya afya Susan Mochache amesisitiza kuwa chanjo ya corona inatolewa bila malipo katika hosipitali zote nchini pamoja na zile za kibinafsi.

Mochache aidha ametoa onyo kali kwa wale ambao watapatikana wakikuka sheria haswa wanasiasa huku akiamuru idara ya DPP kuwachukulia hatua kali za kisheria madakatari waliopatikana wakiuza chanjo ya korona.

Mochache aidha amezisihi hospitali za kibinafsi kusaidia serikali katika kutoa chanjo hiyo kwa wananchi, ili waweze kuendelea na huduma zao za kikazi.

Amesema kufikia sasa takriban watu saba wamekamtwa kwa kuhusika na uuzaji wa chanjo hiyo kinyume cha sheria mmoja wao akiwa ni daktari akisema watafunguliwa mashtaka.

Chanjo za corona takriban milioni 4.5 zinatarajiwa kuwasilishwa humu nchini kufikia kati kati ya mwezi huu wa September, huku serikali ikilenga kuwachanja watu milioni 10 kufikia mwishoni mwa mwezi desemba.

Haya yanajiri huku serikali ya kaunti ya Mombasa ikitarajiwa kuanza kutoa chanjo aina ya moderna kwa watu wazima baada ya kupokea dozi elfu 11 za chanjo hiyo hapo jana.

BY NEWS DESK