HabariNewsSiasa

Waiguru asema jubilee imepoteza umaarufu eneo la kati…….

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru ameendeleza shutma dhidi ya tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kwa kukiuka jukumu lake na kumuandamana visivyo.

Waiguru amesema kwamba hana tatizo akialikwa vikao vya kuhojiwa na EACC ila anakosoa namna tume hiyo imekuwa ikiendesha shughuli zake ikilenga kupata umaarufu.

Kauli hii inajiri siku tatu tuu baada ya Waiguru kudai kwamba makachero wa EACC walivamia makaazi yake kufuatia kauli yake kwamba eneo la kati ya nchi litaangazia upya muelekeo wake wa kisiasa, kabla ya uchaguzi mkuu ujao baada ya mchakato wa BBI kuharamishwa mahakamani.

Akihojiwa na runinga moja humu nchini Waiguru amesema kwamba chama cha jubilee kimepoteza umaarufu kwenye eneo la kati na kusisitiza haja ya chama hicho kuweka mikakati zaidi ya kukikoa kuelekea uchaguzi mkuu.

Waiguru ambaye awali alisema yuko tayari kujiunga na chama chochote kile, amesema iwapo uchaguzi mkuu utafanyika leo basi huenda akawa na wakati mgumu kuwashawishi watu wa eneo hilo kumpigia kura kupitia jubilee.

Inasemekana kwamba huenda Waiguru akajiunga na chama cha UDA ili kutetea kiti chake kufuatia tetesi kwamba katibu katika masuala ya ndani ya nchi dkt Karanja Kibicho huenda akapendelewa na jubilee na kupewa tiketi ya kuwania ugavana.

BY NEWS DESK