HabariNews

EPZ kujengwa huko Golini mjini Voi…..

Bunge la kitaifa limesema sasa litatenga fedha kwa ujenzi wa halmashauri ya EPZ yaani eneo la kutengeneza bidhaa za kuuzwa nje ya nchi yaani export processing zone, katika eneo la Voi.

Akizungumza katika mkutano na baraza la wananchi huko Voi kuhusu mpango wa ujenzi wa kiwanda hicho, mbunge Jones Mlolwa ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya biashara, viwanda na vyama vya ushirika bungeni amesema serikali ya kitaifa inaunga mkono ujenzi wa kiwanda hicho cha EPZ eneo hilo la Voi.

Haya yanajiri huku wakaazi wakitaka kupewa kipau mbele wakati wa mradi huo.

BY NEWS DESK