HabariMazingiraNews

Idara ya mipango maalum yalaumiwa Tanariver kwa ukosefu wa maji…..

Kaimu spika wa bunge la kaunti ya Tana River Sadam Hussein ameishtumu idara ya mipango maalum katika eneo hilo kwa kile anachokitaja kama kuzembea wakati huu ambapo wakaazi wa eneo hilo wanakubwa na makali ya njaa na ukosefu wa maji.

Kulingana na Hussein, idara hio ndio iko na maukumu ya kushughulikia adhari zote za majanga japo, hadi kufikia sasa idara hio imesalia kimya huku akimtaka gavana wa kaunti hio kuingilia kati na kuzungumzia swala hilo.

Hapo jana, maafisa wakuu katika idara hio waliitwa mbele ya bunge na kupewa makataa ya siku mbili kuhakikisha kwamba idara yake inaanza mara moja mipango ya kutoa chakula cha msaada kwa waathiriwa.

BY NEWS DESK