HabariNews

Wafanyi biashara wa soko la konamsa katika kaunti ya Kwale wanakadiria hasara…

Wafanyi biashara wa soko la konamsa katika kaunti ya Kwale, wanakadiria hasara ya mamilioni ya fedha baada ya moto kuzuka na kuteketeza bidhaa zao usiku wa kuamkia leo.

Inadaiwa kuwa moto huo umesababishwa na mabomu ya petrol yaliyorushwa na watu wasiojulikana .

Moto huo umeteketeza vibanda vyote vya kibiashara huku baadhi ya walioathirika wakiilaumu serikali hiyo ya Kwale kwa kushindwa kuzima moto huo kufuatia ukosefu wa magari ya kuzima moto .

BY NEWS DESK