HabariMombasaNews

Joho ni kiongozi wa hivi punde kupinga mpango wa bottom up economic model….

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho amekuwa kiongozi wa hivi punde kupinga mpango wa naibu rais William Ruto wa kuimarisha uchumi wa bottom up economic model.

Kulingana na gavana Joho, Ruto ana malengo ya kibinafsi haswa ya kujinufaisha kisiasa na wala sio kwa manufaa ya wakenya.

Amesema kuna haja ya mikakati inayofanywa kuwekwa wazi kabla ya hatua yoyote ya kuanza kufanikisha uchumi kuanza kutekelezwa.

BY NEWS DESK