HabariNews

Serikali ya kaunti ya Kilifi imehimizwa kuongeza pesa za ufadhili wa masomo……….

Serikali ya kaunti ya Kilifi imehimizwa kuongeza pesa za ufadhili wa masomo unaotolewa kwa wadi ili kutosheleza mahitaji ya wanafunzi.

Kulingana na Mwamutsi, tangu serikali ya kaunti ichukue uongozi chini ya gavana wa Kilifi Amason Kingi kiwango hicho bado kimesalia shilingi milioni 350 kila mwaka hali ambayo imewanyima wengi nafasi ya kupata usaidizi wa kimasomo kutoka kwa serikali hiyo.

Amesema hali hii imechangia wazazi wengi kupitia wakati mgumu kutafuta pesa za karo ili kuwasomesha wanao.

Aidha Mwamutsi amesema serikali ya kaunti hiyo imetenga shilingi  milioni 2.5 za kuwafadhili wanafunzi.

Ameongeza kuwa wanafunzi watakao pewa kipaumbele katika ugavi wa pesa hizo za basari ni wale ambao hawajajiunga na shule za upili mpaka kufikia sasa pamoja na wale wanajiunga na vyuo vikuu.

BY NEWS DESK