HabariNews

Waziri Magoha asisitiza kwamba mtaala wa CBC utasalia kuwepo……

Waziri wa elimu proffesa George Magoha amesisitiza kwamba mtaala wa umilisi wa CBC utaendelea kutekelezwa huku akisema watoto shuleni wanaufuruhia mtaala huo.

Akizungumza katika taasisi ya mafunzo ya KICD, Magoha amesema furaha ya wanafunzi hao ni dhihirisho tosha kwamba mtaala huo uko sawa akisema changamoto zinazokabili utekelezaji wa CBC zinapaswa kutatuliwa na wala sio kufutilia mbali mtaala huo.

Wakati huo huo amepongeza gavana wa kwale Salim Mvurya kwa kuhakikisha sekta ya elimu kaunti ya Kwale inaendeshwa ipasavyo.

Amesema walimu wa shule kaunti ya Kwale wanafundisha wanafunzi bila ya malalamishi yoyote.

Awali taasisi ya kukuza mitaala nchini KICD ilikana kuahidi kushughulikia malalamishi ya baadhi ya wazazi kuhusu mtaala wa umilisi wa CBC.

Akihutubu katika taasisi hiyo, katibu katika wizara ya elimu Julius Jwan amepuuza malalamishi ya wazazi kwamba wanafanyishwa mazoezi tele kutokana na mtaala huo akisema kwamba hawajapata malalamishi yoyote kuashiria kwamba wanawao hawasomeshwi ipasavyo.

Aidha Jwan amesema uhusiano katimya wazazi na wanawao wanapofanya mazoezi nyumbani ni muhimu na kuwashauri wazazi kushiriki kikamilifu.

Kwa upande wao wawakilishi wa tume ya kuajiri walimu TSC wameregelea kauli yao ya awali kwamba iliwapa walimu elfu 228 mafunzo kuhusu mtaala huo wa CBC.

Aidha wamesema mafunzo zaidi kwa walimu elfu 60 wa shule za upili yanatarajiwa kuanza kati ya mwezi machi na aprili mwaka ujao ili kuwatayarisha kwa wanafunzi watakaokuwa wanajiunga na shule za upili.

Aidha wamepuuza tetesi kwamba walimu hao wa grade ya 1 hadi 5 hawanauwezo wa kufanikisha kutekelezwa kwa mtaala huo.

BY NEWS DESK